Photos: Uhuru Kenyatta ampisha Bahati kiti cha Urais

0
19

Siku ya jana Jumamosi tarehe 10/9/2016 kulitimka kitimtim katika uwanja wa Kasarani. Ilikuwa ni siku maalum kwa wakenya wakiongozwa na vinara wa mrengo wa Jubilee wakati wakizindua chama kipya cha Jubilee baada ya kuvunja vyama vingi vidogo vya kisiasa na kuungana kwa chama hicho kipya. Mwimbaji wa Gospel, Kelvin Bahati alifanya ya kwake wakati alipopata fursa ya kutumbuiza umati mkubwa uliokuwa umehudhuria mkutano huo. Ama kweli ilikuwa ni siku ya “Bahati” kuweza kupata nafasi ya kukalia kiti cha rais Uhuru Kenyatta huku akiwashangaza wageni waalikwa kwa kumwacha hoi Kenyatta akiwa amesimama tu bila cha kufanya. Bahati alitumbuiza kwa nyimbo zake tamu ikkwemo ‘Mama’ wimbo aliomwimbia mama wa taifa Bi. Margaret Kenyatta. Umati ulimshangilia kwa furaha sana mwimbaji Bahati kuweza kufanya kitendo hicho mbela za hadhira kwa kumpokonya urais Uhuru japo kwa muda mchache tu. Wengine walikejeli hatua hio kwa kumsuta Bahati kwenye mitandao ya kijamii. TUZIDI KUUKUZA MUZIKI WA KWETU.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY