Daddy Q Atiwa Mbaroni

0
15

Mapema hii leo, msanii mkongwe wa mziki aina ya dancehall kutoka Mombasa ametiwa mbaroni na maafisa wa traffic. Msanii huyo ambaye alikua ametoka kuwachukua wanawe kutoka shule ya bweni wanayosomea mjini Eldoret akielekea jijini Nairobi anakoishi ametiwa mbaroni na maafisa wa NTSA (National Transport and Safety Authority) kwa kosa la kuendesha gari kwa kasi. Daddy Q, alikua anaendesha gari lake kwa spidi ya 100km/h na akaongeza mwenda alipokua aki,overtake trailer hadi mwendo wa 112km/h. Asilojua ni kwamba maafisi wa NTSA walikua wakifuatilia mwendo wake kabla kumsimamisha eneo la Sachangwany, Molo ambapo amebikwa breki na maafisa hao na kumtia mbaroni kwa kosa hilo. ‘Nilitakiwa nilipe Kshs.10,000 ili tuachiwe huru alafu tuandikiwe barua ya kuenda kortini. Hio nimeona ni kunyanyaswa ikabidi nipigie jamaa zangu ambao wana usemi ndio wakawapigia simu maafisaa hao waliokua wametukamata. Mwishome nimetoa tu Kshs.5000 alafu tukaachiwa huru na ndio tukawa tumemmalizana..hakuna cha mammbo na kortini wala nini’ Daddy Q amenieleza huku akisema ya kwamba wako salama salmin hata wanakaribia kufika jijini Nairobi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY