Msanii Kutoka Mombasa Atimiza Sharti Alilopewa Na WCB Wasafi Kabla Kufanya Kazi Nao

0
17

Kabla Diamond Platinumz kuenda nchini Marekani ku,shoot video ya collabo yake na superstar wa kimataifa, mkali wa rnb, NEYO, Diamond alikua humu mjini Meru ambapo alifanya show moja kubwa sana. Kama vilevile ambavyo management ya Diamond ilivyotumia fursa ya Neyo kuja nchini Kenya kwa ajili ya Coke Studio na kufanya mazungumzo na kuwahi collabo na msanii huyo wa Amerika, pia management ya msanii Jay Madini ilichukua fursa hio ya ujio wa Diamond na management yake ya WCB kuweza kupanga kufanya kazi kati ya Jay Madini na management hio ambayo kwa sasa ndio inatamba Afrika Mashariki. Young Boss Music, ambayo ndio inamsimamia Jay Madini ilifanikiwa kukubaliana na WCB kum’wezesha Jay Madini kufanya kazi na label hio kubwa. Ijapokua management ya YoungBoss ilikataa kueleza kwa kina kuhusu makubaliano hayo…yani kama ni collabo na ni kati ya msanii yupi wa WCB na Jay Madini au ni kwamba alikua ata,signiwa katika label hio, walichoweza kudokeza ni kwamba kati ya vigezo walivyopewa ni kwamba Jay Madini afanye video moja kubwa kwanza ambayo gharama yake isiwe chini ya Kshs. 1,000,000. ‘Kile kikubwa tulichokua tumeambiwa tukifanye kabla Jay kufanya kazi na WCB tumekifanya, ilichobaki ni kupanga tarehe tu ya kuandikishana mkataba na WCB’ Ameeleza Morris Mbetsa ambaye ndio mmiliki wa YoungBoss Music, kampuni ambayo inasimamia wasanii nchini Kenya, Tanzania, Africa Kusini na Nigeria ameeleza zaidi jinsi walivyochukulia kwa uzito video hioo kwani iliwabidi hadi kusafirisha model kutoka nchini Ujerumani.

Itazame video hio hapa chini…..

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY